Asili na mazingiraAzerbaijan
Ulaya: Tutaongoza juhudi za kuzisaidia nchi masikini
18 Novemba 2024Matangazo
Hoekstra, amesema hayo leo Jumatatu na kuongeza kuwa nchi zote tajiri zinazochafua hewa zina wajibu wa kutoa mchango wao.
Umoja wa Ulaya ndiye mchangiaji mkubwa wa fedha za kusaidia nchi maskini kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, lakini unataka mataifa makubwa kama China pia kuchangia.
Nchi zinazoshiriki mkutano wa kukabili mabadiliko ya tabia nchi wa COP29 mjini Baku Azerbaijan, zinapaswa kupata mkataba mpya, kupiga jeki juhudi za kupambana na athari za tabia nchi katika nchi maskini.
Lakini mazungumzo hayo yamekwama kuhusu nani anapaswa kulipa, kwa kiwango gani na taratibu za mkataba wowote upya wa ufadhili.