Umoja wa Ulaya umeiongezea vikwazo Myanmar
22 Juni 2021Hatua hiyo iliyosainiwa na mawaziri wa mambo ya nje wanaokutana Luxemburg inalenga sekta ya vito na sekta ya maliasili. Taarifa ya Umoja wa Ulaya iliyotangaza hatua hiyo imesema kusudio lao ni kulizuia jeshi kufaidika na maliasili ya Myanmar.
Watu walioorodheshwa ni pamoja na mawaziri na naibu mawaziri, na mwanasheria mkuu - wanaotuhumiwa kudhoofisha demokrasia na utawala wa sheria kwa kukiuka haki za binadamu. Kwa ujumla vikwazo vya Umoja wa Ulaya hadi sasa vinawalenga watu 43 na makampuni sita. Uingereza iliyawaka katika orodha ya vikwazo makampuni mengine matatu ya taifa hilo Jumatatu ya juma lililopita.
Urusi inalalamikiwa kwa kuunga mkono utawala wa kijeshi wa Myanmar.
Katika hatua nyingine, huko katika mkutano uliofanyika mjini Moscow, Mtendaji wa Mkuu wa Baraza la Ulinzi la Urusi, na kiongozi wa kijeshi wa Myanmar Min Aung Hlaing, wamekubaliana kuongeza jitihada zao katika kuboresha suala la ulinzi pamoja na mahusoano baina ya Urusi na Myanmar.
Stephane Dujarric ni Msmaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. anasema "Na habari za sasa kutoka Myanmar, kwa zingatio la timu ya uwakilishi ya Umoja wa Mataifa nchini humo, leo inatoa wito wa kuachiwa kwa haraka maelfu ya wanawake, watoto na wanaume ambao wapo kizuizini, ikiwa takribani miezi mitano tangu jeshi lidhibiti nchi Februari Mosi."
Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 5,000 wamewekwa kizuizini.
Aidha mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa amesema ameongeza kwa kusema "Kwa mujibu wa ofisi ya haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa hadi wakati huu idadi ya waliokamatwa na kuwekwa kizuizini inapindukia 5,000. Kwa nyongeza, karibu watu 2,000 wakiwemo wanasiasa, waandishi vitabu, watetezi wa haki za binaadamu, watoa huduam za afya, waandishi wa habari pamoja na wanachi wakawaida wanaishi kwa kujificha kutokana na kutolea kwa waranti ya kukamatwa kwao."
Makundi ya haki za binaadamu, yamekuwa yakiituhumu Urusi kwa kuupa uhalali uongozi wa kijeshi wa Myanmar kwa kuendelea kufanya ziara za ushirikiano na kuingia makubaliano ya silaha. Lakini Urusi kwa upande wake imekuwa ikisema ina uhusiano wa muda mrefu na Myanmar.
Hadi wakati huu, si vikwazo, diplomasia wala maaandamano ambavyo vimeweza kuurejesha utawala wa kijeshi katika mstari wa kidemokrasia. Kwa mujibu wa makundi ya haki za binaadamu zaidi ya 800 wameuwawa na vikosi vya usalama na wengine 4,500 kufungwa gereza tangu kuzuka kwa vuruigu za baada ya mapinduzi ya kujeshi ya Februari Mosi mwaka huu.
Chanzo: Reuters