1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya na jumuia ya NATo zakubali kusaiadia juhudi za amani za umoja wa Agrika katika jimbo la darfour

24 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFAe

Umoja wa Ulaya uko tayari kusaidia juhudi za amani za umoja wa Afrika katika jimbo la magharibi la Sudan Darfour.Habari hizo zimetangazwa baada ya mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa umoja wa ulaya mjini Brussels.Misaada ya Umoja wa ulaya itahusiana zaidi na shughuli za usafiri wa nchi kavu na angani.Na habari za hivi punde zinasema jumuia ya kujihami ya magharibi NATO nayo pia imetaangaza rasmi utayarifu wake wa kusaaidia juhudi za amani za umoja wa Afrika huko Darfour.Jumuia ya kujihami ya magharibi NATO na Umoja wa Ulaya zimeahidi kushirikiana katika kutoa misaada huko Darfour.Zaidi kuhusu misaada hiyo ,itaajulikana baada ya mkutano wa wafadhili utakaofanyika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia alkhamisi ijayo.Mkutano huo utasimamiwa kwa pamoja kati ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Alpha Oumar Konare.