Umoja wa Ulaya kujadili kuzuia fedha kueleka Hungary
6 Desemba 2022Mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya leo watajadili kuhusu kuzuia kiasi dola bilioni 13 katika hazina ya fedha za bajeti ya Umoja huo na kiasi dola bilioni 5.8 za msaada wa kupambana na Uviko 19 zilizotakiwa kutolekwa kwa Hungary.
Hatua hiyo inachukuliwa kutokana na wasiwasi juu ya utawala wa sheria katika nchi hiyo. Licha ya Hungary kutoa ahadi ya kufanya mageuzi. Halmashauri ya Umoja wa Ulaya ilipendekeza kuzuiwa fedha hizo ukisema juhudi za nchi hiyo za kupambana na rushwa na kuimarisha utawala wa sheria hazitoshi.
Halmashauri hiyo ambayo ndiyo chombo kikuu cha maamuzi hivi sasa kinasubiri matokeo ya mkutano huo utakaofanyika Brussels, kuchukua hatua hiyo. Halmashauri hiyo imesisitiza kwamba hakuna fedha zitakazotolewa kwa Hungary hadi nchi hiyo itakapokamilisha kufanya mageuzi yote yaliyotakiwa.