1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kuipatia Lebanon msaada wa dola bilioni moja

2 Mei 2024

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen yupo ziarani nchini Lebanon na amekutana kwa mazungumzo na waziri mkuu wa muda wa nchi hiyo Najib Mikati pamoja na viongozi wengine mjini Beirut.

https://p.dw.com/p/4fRNj
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen,Rais wa Cyprus Nikos Christodoulides, Spika wa Lebanon Nabih Berri mjini Beirut.
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen,Rais wa Cyprus Nikos Christodoulides wakiwa na Spika wa Lebanon Nabih Berri mjini Beirut.Picha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Von der Leyen ambaye ameambatana na Rais wa kisiwa cha Cyprus Nikos Christodoulides ametangaza kuwa Umoja wa Ulaya utaipatia Lebanon msaada wa euro bilioni 1 ili kusaidia kukuza uchumi wa taifa hilo lakini pia kuimarisha uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Lebanon.

Waziri Mkuu wa muda wa nchi hiyo Najib Mikati amesema wimbi lolote la watu wanaokimbia makazi yao si tishio pekee kwa Lebanon, bali wimbi hilo litaenea hadi Ulaya na kuwa mgogoro wa kikanda na kimataifa.

Soma pia:Umoja wa Ulaya kuipatia Lebanon msaada wa dola bilioni moja

"Tuna hakika kabisa kwamba usalama wa Lebanon ni usalama wa nchi za Ulaya na kinyume chake."

Lebanon, yenye zaidi ya wakimbizi 800,000 wa Syria wanaoishi katika umasikini mkubwa, imekuwa ikikabiliwa na mgogorowa uchumi tangu mwaka 2019.