1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Umoja wa UIaya wataka ulinzi katika Ujia wa Taiwan

23 Aprili 2023

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ametoa mwito kwa vikosi vya majini vya Umoja huo kufanya doria katika Ujia wa Bahari ya Taiwan.

https://p.dw.com/p/4QSIF
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amehimiza kuulinda Ujia wa BAhari wa Taiwan, ili pia kulinda maslahi yao ya kiuchumi
Kisiwa cha Taiwan kimekuwa kitovu cha mvutano hasa kati ya China na Marekani kutokana na maslahi ya kila nchini.Picha: Frederick Florin/AFP via Getty Images

Borrell ametoa mwito huo na kuongeza kuwa hatua hiyo italenga kudhihirisha wajibu wao katika suala zima la usalama wa kisiwa hicho.

Borrell amesema hayo katika maoni yaliyochapishwa hii leo kwenye gazeti la wiki la Ufaransa la Du Dimanche.

Awali alitoa matamshi kama hayo katika bunge la Ulaya, wakati wa mjadala kuhusu China. Amesema kimsingi Taiwan ni sehemu ya eneo lao la kimkakati linalotakiwa kuhakikishiwa usalama, na sio tu kwa sababu ya maadili bali pia kutokana athari za kiuchumi kwa kuwa eneo hilo ni muhimu sana katika uzalishaji wa vifaa vinavyotumiwa kutengeneza bidhaa za kielektroniki.

China inayodai Taiwan ni sehemu ya himaya yake, haijaondoa uwezekano wa kutumia nguvu ili kukidhibiti kisiwa hicho.