Umoja wa Mataifa watoa tahadhari ya njaa Haiti na sudan
29 Mei 2023Matangazo
Kulingana na mashirika ya chakula na kilimo ulimwenguni, FAO pamoja na Mpango wa chakula, WFP, Ukanda huo wa Sahel, Sudan na Haiti unaungana na mataifa mengine ambayo bado yanatishiwa na balaa hilo ambayo ni Burkina Faso, Mali, Afghanistan, Nigeria, Sudan Kusini na Yemen.
Ripoti ya mashirika hayo mawili imesema hali hiyo imechochewa na vizuizi vikali vilivyowekwa na wanamgambo wa jihadi, vya watu kutembea na kusafirisha bidhaa nchini Burkina Faso na Mali, mzozo wa kiusalama nchini Haiti na mapigano yaliyozuka nchini Sudan.
Ripoti hiyo aidha, imeangazia hatari iliyopo ikiwa mzozo huo wa Sudan utazidi kusambaa pamoja na hofu inayoibuliwa na uwezekano wa mvua za El Nino dhidi ya mataifa yaliyo hatarini zaidi.