1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa wataka mkutano wa dharura kwa ajili ya Somalia

22 Julai 2011

Umoja wa mataifa umetoa wito wa kufanyika mkutano wa dharura mjini Rome wiki ijayo kuweza kupata msaada kwa ajili ya mataifa ya Afrika mashariki.

https://p.dw.com/p/121UI

Umoja wa mataifa umetoa wito wa kufanyika mkutano wa dharura mjini Rome wiki ijayo ili kuweza kupata msaada kwa ajili ya mataifa ya Afrika mashariki. Umoja wa mataifa umetangaza kuwapo kwa baa la njaa la kwanza duniani katika miaka 20 kusini mwa Somalia. Mpango wa chakula duniani umetangaza mipango ya kuanza kupeleka msaada wa chakula kwa ndege nchini Somalia katika muda wa siku chache zijazo. Mzozo wa kivita umezuwia upelekaji wa chakula . Watu wanaokadiriwa kufikia milioni 12 wanapambana na njaa kali katika hali mbaya kabisa ya ukame katika eneo la pembe ya Afrika kuwahi kuonekana katika muda wa miaka 60. Kila siku , maelfu ya watu wanavuka mpaka kutoka nchi ya Somalia inayokabiliwa na ukame na kuingia Ethiopia na Kenya wakitafuta chakula. Kambi za muda katika nchi hizo zimefurika watu na chakula kinapungua.