Umoja wa Mataifa wataka mabadiliko baraza la usalama
21 Mei 2023Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa Antonio Guterres leo hii amesema umewadia wakati wa kulifanyia marekebisho Baraza la Usalama pamoja na mfumo wa ubadilishaji wa fedha ulimwenguni ujulikanao kama "Bretton Woods" ili viendanane na hali ya ulmwengu wa sasa.Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Hiroshima, Japan, unakofanyika mkutano wa kilele wa kundi la mataifa 7 tajiri, Guterres amesema taasisi zote mbili zimekuwa zikiakisi mahusiano ya kimamlaka ya mwaka 1945, hivyo zinahitaji maboresho.Amesema mfumo wa kifedha wa kimataifa umepitwa na wakati na hauna usawa. Kutokana na matukio ya ghafla ya janga la UVIKO-19 pamoja na uvamizi wa Ukraine, umeshindwa kutimiza majukumu yake ya msingi kimataifa.