1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wataka Georgia kuondoa mswada kandamizi

3 Mei 2024

Mkuu wa ofisi ya haki ya Umoja wa Mataifa Volker Turk ametoa wito kwa serikali ya Georgia kuondoa mswada wenye utata ulio katika mchakato wa kibunge na kuelezea wasiwasi wake kuhusu ukandamizaji wa polisi kwa umma.

https://p.dw.com/p/4fSAe
Maandamano dhidi ya mswada wa "ushawishi wa kigeni" huko Georgia
Maandamano dhidi ya mswada wa "ushawishi wa kigeni" huko GeorgiaPicha: Vano Shlamov/AFP

Kauli yake imekuja siku moja baada ya bunge la Georgia kupitisha rasimu ya sheria hiyo kusomwa kwa mara ya pili na siku nyingine ya maandamano dhidi ya mswada huo, ambao wakosoaji wanasema ni jitihada za kuwanyamazisha wapinzani.

Katika taarifa yake Turk ameitaka serikali ya Georgia kuweka kando mara moja na kuanzisha mjadala shirikilishi, wenye kuzihusisha asasi za kiraia na vyombo vya habari.

Iwapo utapitishwa, sheria yake itahitaji asasi ya kiraia yoyote na vyombo vya habarivinayopokea zaidi ya asilimia 20 ya ufadhili wake kutoka nje ya nchi visajiliwe kama taasisi zinazopigia chapuo maslahi ya taifa la kigeni.