1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa waionya Libya kutumbukia kwenye mgawanyiko

16 Februari 2024

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Abdoulaye Bathily, amewaonya viongozi hasimu kwamba ikiwa hawataunda serikali ya umoja na kuelekea kwenye uchaguzi, nchi hiyo itatumbukia katika mgawanyiko.

https://p.dw.com/p/4cSxu
Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Abdoulaye Bathily.
Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Abdoulaye Bathily.Picha: Yousef Murad/AP Photo/picture alliance

Bathily aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba kuna dalili nyingi za kutisha za kutokea kwa mgawanyiko huo na aliwataka viongozi wote wa kisiasa kuweka kando "maslahi yao binafsi" na kukaa kitako kufanya mazungumzo na kufikia maelewano kudumisha hadhi ya nchi hiyo.

Soma zaidi: Umoja wa Mataifa waonya kuhusu machafuko Libya

Bathily aliongeza kuwa kusita kufanya hivyo kunatilia mashaka sio tu kujitolea kwao katika uchaguzi, lakini pia kwa umoja na mustakabali wa nchi hiyo.

Bathily aliliambia Baraza hilo kuwa katika mazungumzo yake ya hivi karibuni na wadau wakuu, hakuna aliyebatilisha msimamo wa awali na kila mmoja ameweka masharti ya kushiriki katika mazungumzo ya kutatua masuala yanayozozaniwa, ambayo huenda yakafungua njia kwa uchaguzi unaosubiriwa kwa muda mrefu.