Umoja wa Mataifa wahofia vifo vya watoto Sudan
25 Agosti 2023Matangazo
Afisa mwandamizi katika Umoja wa Mataifa na mratibu wa misaada ya kiutu, Martin Griffiths, amesema, vita vya Sudan vinachochea hali kubwa ya dharura ya kiutu.
Sooma zaidi: Burhan aonekana kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita
Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, katika kipindi cha miezi minne iliyopita tangu mapigano ya Sudan yaanze, watu 5,000 wameuwawa na milioni 4.6 kulazimika kuyakimbia makaazi yao.