1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaSudan

Umoja wa Mataifa : Visa vya kipindupindu vyaongezeka Sudan

9 Oktoba 2024

Visa vya ugonjwa wa kipindupindu Sudan vimeongezeka kwa karibu asilimia 40 chini ya kipindi cha wiki mbili wasema Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4laA6
Visa vya ugonjwa wa kipindupindu Sudan vimeongezeka kwa karibu asilimia 40 chini ya kipindi cha wiki mbili
Visa vya ugonjwa wa kipindupindu Sudan vimeongezeka kwa karibu asilimia 40 chini ya kipindi cha wiki mbili Picha: AFP/Getty Images

Takwimu hizo za hivi karibuni zimesababisha wasiwasi kwa maafisa wa afya wa Umoja wa Mataifa ambao kwa muda mrefu wameonya kuhusu mripuko huo, na kukosekana kwa njia sahihi za kupambana nao tangu uliporipotiwa mwezi Julai.

Wizara ya Afya ya Sudan ilisema mapema Jumatatu kuwa karibu visa 21,288 viliripotiwa kwenye majimbo 11 kati ya 18 katika kipindi hicho pamoja na vifo 626.

Visa vingi vya maambukizi vilikuwa katika mji wa Kassala ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto, UNICEF linashirikiana na wizara ya afya na Shirika la Afya Duniani, WHO katika kutoa awamu ya pili ya chanjo ya matone ya kipindupindu iliyoanza mwezi uliopita.