1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa, New York. Mwendesha mashtaka kutoka Ujerumani, kuchunguza kifo cha waziri mkuu wa zamani wa Lebanon , Bwana Hariri.

14 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFDk

Umoja wa mataifa umemteua mwendesha mashtaka kutoka Ujerumani ili kuchunguza mazingira yaliyopelekea kifo cha waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri. Detlev Mehlis ni mwongoza mashtaka mkuu katika ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali mjini Berlin. Ana uzoefu mkubwa katika kuchunguza uhalifu wa kimataifa na kigaidi, ikiwa ni pamoja na uchunguzi alioufanya kufuatia shambulio la bomu la mwaka 1986 katika ukumbi wa disco mjini Berlin.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeamuru uchunguzi ufanywe na umoja wa mataifa kuhusiana na kifo cha Bwana Hariri baada ya kuona kuwa uchunguzi uliofanywa na serikali ya Lebanon haukuwa sahihi. Wengi wanadhani kuwa Syria inahusika na kifo hicho kilichotokea Februari mwaka huu.