UN: yapiga kura kushinikiza kusitishwa mapigano Gaza
25 Machi 2024Matangazo
Kura hiyo itapigwa baada ya siku ya Ijumaa Urusi na China kutumia kura zao za turufu kupinga azimio lililoandaliwa na Marekani kuhusu kusitishwa mapigano kwenye mzozo kati ya Israel na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Marekani imetahadharisha kwamba kura itakayopigwa inaweza kuathiri makubaliano ya kumaliza mvutano yaliyoratibiwa na taifa hilo pamoja na Misri na Qatar, hali inayoibua wasiwasi wa kura nyingine ya turufu kutumiwa na Marekani.
Israel yazingira hospitali mbili zaidi zilizoko mji wa Khan Younis
Azimio hilo, lililowasilishwa na wajumbe 10 wa kuchaguliwa wa Baraza la Usalama linaungwa mkono na Urusi na China na mataifa 22 ya Kiarabu kwenye Umoja wa Mataifa.