1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika wautaka Umoja wa Mataifa kwenda Somalia

Josephat Nyiro Charo27 Julai 2010

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika watarajiwa kumalizika leo Kampala, Uganda

https://p.dw.com/p/OVQG
Wakuu wa nchi za Umoja wa AfrikaPicha: AP

Mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika unatarajiwa kumalizika leo katika mji mkuu wa Uganda, Kampala. Katika kikao cha jana kilichofanyika hadi usiku, baadhi ya marais wanachama wa umoja wa Afrika wanautaka umoja wa mataifa kwenda Somalia na kuchangia kwenye juhudi za kuleta amani badala ya kusema utasaidia umoja wa Afrika kutekeleza jukumu hilo.

Mwandishi: Leyla Ndinda

Mhariri: Josephat Charo