1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

AU sasa ni mwanachama wa kudumu wa kundi la G20

9 Septemba 2023

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, ameutangaza Umoja wa Afrika kuwa mwanachama wa kudumu wa kundi la mataifa tajiri na yale yanayoinukia kiuchumi la G20

https://p.dw.com/p/4W8mS
Waziri mkuu wa India Narendra Modi akihutubia mkutano wa G20 nchini India
Waziri mkuu wa India Narendra Modi

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Modi, aliualika Umoja wa Afrika unaowakilishwa na mwenyekiti wake Azali Assoumani kuchukuwa nafasi yake katika kundi hilo kama mwanachama wa kudumu. Modi ameongeza kuwa hatua hiyo italiimarisha kundi hilo na nchi zenye viwango vya chini vya kiuchumi na maendeleo.

Umoja wa Afrika sasa una hadhi sawa na Umoja wa Ulaya

Umoja wa Afrika wenye mataifa wanachama 55, sasa una hadhi sawa na Umoja wa Ulaya, kundi la pekee la kikanda lenye uanachama wa kudumu katika G20. Hadhi yake ya awali katika G20, ilikuwa shirika la kimataifa lililoalikwa.