1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulinzi mkali waimarishwa mjini Maputo kuelekea maandamano

7 Novemba 2024

Majeshi na polisi leo wameonekana wakipiga doria katika mitaa ya mji mkuu wa Msumbiji, Maputo, kuelekea maandamano yaliyopangwa kupinga matokeo ya uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4mjzR
Hali ilivyo mjini Maputo
Hali ilivyo mjini Maputo Picha: Alfredo Zuniga/AFP/Getty Images

Majeshi na polisi leo wameonekana wakipiga doria katika mitaa ya mji mkuu wa Msumbiji, Maputo, kuelekea maandamano yaliyopangwa kupinga matokeo ya uchaguzi ambao upinzani umeutaja kama uliokumbwa na udanganyifu. Mji huo mkuu ulio na idadi ya zaidi ya watu milioni moja, ulikuwa mtulivu bila heka heka zozote asubuhi ya leo huku maduka, benki, shule na vyuo vikuu vikifungwa.Mamlaka Msumbiji zatishia kutumia jeshi kudhibiti maandamano

Mgombea wa upinzani, Venancio Mondlane, ambaye anaamini kwamba alishinda uchaguzi huo, alikuwa ameitisha maandamano makubwa nchini humo hii leo. Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kuwa karibu watu 18 wameuwawa katika machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi huo. Lakini shirika lisilo la kiserikali nchini humo la Kituo cha Demokrasia na Haki za Binadamu, CDD, limesema kuwa idadi ya waliofariki ni watu 24.