1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulimwengu waadhimisha Siku ya Haki za Binaadamu

10 Desemba 2015

Umija wa Mataifa unasema maudhui ya mwaka huu kuhusu uzinduzi wa kampeni itakayodumu mwaka mzima ya kusherehekea miaka 50 ya mikataba miwili ya zamani kabisa ya kimataifa kuhusu haki za binadamu

https://p.dw.com/p/1HL6z
Guantanamo Camp 4 Symbolbild CIA Folterprogramm
Picha: picture-alliance/ZUMA Press

Mkataba wa Kimataifa Kuhusu Haki za Kiraia na Kisiasa na Mkataba wa Kimataifa kuhusu Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni.

Nakala hizi mbili, pamoja na Azimio la Haki za Binaadamu Ulimwenguni, kutoka kwa Mswada wa Kimataifa wa Haki za Binaadamu, ambazo pamoja ziliunda haki za kiraia, kitamaduni, kiuchumi, kisiasa na kijamii ambazo ndio msingi wa wanadamu wote.

Kanuni zilizopo kwenye nakala hizo zinauhusu ulimwengu mzima. Zinamhusu kila mmoja, kila mahali aliko. Hiyo ina maana kuwa mienendo ya kitamaduni na kijamii haiwezi kuhalalisha kuondolewa kwa kanuni hizo. Uhuru huu unajumuisha uhuru wa kuepukana na hofu, uhuru wa mawazo na kidini.

Combobild Amnesty International und Human Rights Watch Logos
Mashirika ya Kutetea Haki za Binaadamu yako mstari wa mbele kupinga ukiukwaji wa hakiPicha: picture-alliance/dpa, Getty Images

Ulimwengu umebadilika tangu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliidhinisha Mikataba hiyo miwili mwaka wa 1966. Mikataba hiyo pamoja na mikataba mingine ya haki za binaadamu, imetekeleza jukumu muhimu la kuhakikisha kuwa kuna heshima na utambuzi katika kipindi cha miongo mitano ambayo mara nyingine imekuwa na misukosuko.

Katika kuadhimisha siku ya haki za binaadamu dunani Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International leo limetoa mwito wa kuyashughulikia mambo yanayosababisha ukimbizi na limezitaka nchi ziwapokee wakimbizi kwa namna ambavyo mwanadamu anastahili.

Akizungumza mjini Berlin, katibu mkuu wa asasi hiyo, tawi la Ujerumani, Selmini Caliskan amesema kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kunaonekana wazi katika mgogoro wa nchini Syria uliosababisha mamilioni ya watu wageuke wakimbizi.

Asasi hiyo ya kutetea haki za binadamu pia imezikosoa baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya kwa kujenga kuta ili kuwazuia wakimbizi, lakini wakati huo huo zinaimarisha ushirikiano na nchi zinazokiuka haki za watu wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi. Amnesty International imeitaka jumuiya ya kimataifa, hadi mwishoni mwa mwaka ujao, iwape hifadhi watu laki nne, kutoka Syria na Mashariki ya Kati kwa jumla, ambao hasa wanahitaji hifadhi ya ukimbizi.

Mwandishi: Bruce Amani/UN/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman