1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yakumbwa na matokeo mabaya ya hali ya hewa

8 Agosti 2023

Ulaya inakumbwa na matokeo mabaya ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na mafuriko, mamia ya maporomoko ya udongo, wimbi la joto na mioto ya nyika.

https://p.dw.com/p/4UtG7
Slovenia
Athari za mafuriko SloveniaPicha: Fedja Grulovic/REUTERS

Ulaya inakumbwa na matokeo mabaya ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na mafuriko, mamia ya maporomoko ya udongo, wimbi la joto na mioto ya nyika. Vifo sita vimeripotiwa huku waokoaji wakiendelea kupambana na matukio hayo katika mataifa ya Slovenia, Austria na Croatia.

Soma pia: Ugiriki yapambana na mioto mikubwa ya msituni

Mamlaka nchini Slovenia wamearifu kuwa mafuriko yameathiri theluthi mbili ya wakazi milioni 2.1 na Waziri Mkuu wa Slovenia Robert Golob amekadiria kuwa hasara iliyotokana na mafuriko hayo imefikia Euro milioni 500 na ameomba msaada wa haraka kutoka Jumuiya ya Kimataifa.

Nchini Austria, zaidi ya maporokomo 80 ya udongo yameripotiwa wakati kwenye taifa jirani la Croatia hali ya tahadhari imetangazwa katika baadhi ya majimbo kutokana na kitisho cha kutokea maafa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Wimbi la joto limeendelea kushuhudiwa katika mataifa ya Uhispania, Ugiriki na Ureno.