Maafisa wa juu wa Umoja wa Ulaya walipambana kuuza mpango wao mpya wa kuifanyia mageuzi sera ya uhamiaji na wakimbizi. Wakati mashirika ya haki za binadamu yameukosoa umoja huo kwa kutafuta kuziridhisha serikali zinazopinga uhamiaji, hasa kutoka upande wa mashariki, kundi la viongozi wa mataifa ya mashariki limeyakataa mapendekezo hayo.