Ukuta kujengwa Lamu kuwazuia magaidi
13 Machi 2015Matangazo
Gavana wa Kaunti ya Lamu nchini Kenya, Issa Timammy, amezua mjadala kuhusu mpango wa serikali ya kaunti yake kujenga ukuta kwenye mpaka wa Kenya na Somalia katika juhudi za kukabili ugaidi. Akiuhutubia umma katika ukumbi wa Faza mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu wa 2014 Gavana Timammy alisema ukuta huo wa kilomita thelathini hivi utajengwa kati ya mji wa Ishakani na Ras Kamboni, ambapo mashambulizi ya ugaidi yalishuhudiwa mwezi Julai mwaka jana na kusababisha vifo vya watu takribani 90.
Geoffrey Mung'ou alimhoji Gavana Timammy ambaye alianza kwa kueleza ukuta wenyewe ni wa aina gani hasa.
Kusikiliza mahojiano haya bonyeza alama za spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Geoffrey Mung'ou
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman