1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine:Urusi yapambana kukamata udhibiti kamili Bakhmut

Hawa Bihoga
29 Machi 2023

Vikosi vya Urusi vimeendelea na majaribio ya kuchukua udhibiti kamili wa miji ilioshambuliwa kwa mabomu ya Bakhmut na Avdiivka mashariki mwa Ukraine,duru za kijeshi zinasema hawakufikia lengo,baada ya kurudishwa nyuma.

https://p.dw.com/p/4PPju
Ukraine Krieg | Wolodymyr Selenskyj in Bachmut
Picha: Ukrainian Presidency/AA/picture alliance

Miji hiyo miwili pamoja na mingine ya karibu ikiwemo eneo la viwanda la Donetski imeendelea kushuhudia mkururo wa mashambulizi ya vikosi vya Urusi.

Jeshi la Ukraine upande wa masharikilimesema katika taarifa yao siku ya Jumanne usiku kwamba, wamerekodi visa takriban 70 vya mashambulizi ya makombora huko katika mji wa Bakhmut pekee.

Taarifa hiyo imeendelea kuongeza kwamba wanajeshi wa Ukraine walifanikiwa kurudisha nyuma vikosi vya Urusi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ambae amefanya ziara ya kikazi eneo la Kaskazini-Mashariki la Sumy na kuupa hadhi mji wa Okhtyrka  kama "mji wa kishujaa" kutokana na kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Zelensky amesema eneo la mpakani linarejea kwenye maisha ya kawaida licha ya kuwa kwenye mpaka na Urusi na kushuhudia mashambulizi ya mara kwa mara ya vikosi vya Moscow.

"Eneo lipo karibu na adui.Vitisho ni mara kwa mara.Mashambulizi ni mara kwa mara." Alisema katika hotuba yakeikiwa ni utaratibu wa kila siku.

Katiba hotuba yake iliolenga kuelezea maendeleo kwenye uwanja wa mapambano amesema maisha ya watu ni imara kuliko hofu yoyote.

Soma pia:Vikosi vya Urusi vyabadili mwelekeo wake Bakhmut

Urejeshwaji wa maeneo yaliyotwaliwa unaendelea, biashara inarudi pole pole, na watu wanajenga upya maisha yao. Alisema Zelensyk

"Nilipata heshima ya kuwasilisha jina maalum la jiji la shujaa kwa Okhtyrka."

Hali ya kimaisha katika mji huo ambao ulisaidia kuokoa mashariki na kati ya Ukraine na upinzani wake imeonekana kumridhisha rais Zelensky.

Belarus:Tunajibu vikwazo vya Magharibi

Putin und Lukaschenko | Archivbild 2019
Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Belarus Alexander LukaschenkoPicha: Sergei Chirikov/POOL EPA/AP/dpa/picture alliance

Mshirika wa karibu wa Urusi, Belarus amethibitisha kuwa mwenyeji wa silaha za nyuklia za Urusi akisema kufikiwa kwa uamuzi huo ilikuwa ni jibu kwa vikwazo vya Magharibi na kile ilichokiita kujengwa kijeshi na nchi wanachama waNATO karibu na mipaka yake.

Rais wa Marekani Joe Biden amewaambia waandishi wa habari kuwa kulikuwa na wasiwasi juu ya Kremlin kutekeleza mpango huo wa zana za nyuklia kwa jirani yake Belarus.

Soma pia:Belarus yasema shinikizo la Magharibi limefanya ipokee silaha za nyuklia

Biden katika mkutano wake na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, ameutaja mpango huo kama mazungumzo "hatari".

Amesisitiza kwamba hakuna dalili zozote zinazoonesha kwamba kiongozi huyo atatumia silaha hizo nchini Ukraine.

Ukaguzi wa kwenye mtambo wa nyuklia Zaporizhzhia

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Matumizi ya Nishati ya Nyuklia IAEA,Rafael Grossi atafanya ziarakwenye kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia leo Jumatano.

Kinu hicho kilichopo kusini mwa Ukraine kinadhibitiwa kimkakati na Urusi ambapo mara kadhaa hali imeripotiwa kuwa ni ya wasiwasi katika eneo hilo.

Soma pia:Zelenskiy: Urusi inakishikilia mateka kinu cha nyuklia cha Zaporizhzia

Grossi katika mazungumzo yake na Reuters amesema kwamba, jukumu lake la kuhakikisha kunakuwepo makubaliano ya kulinda kinu hicho kikubwa zaidi cha nishati ya nyuklia barani Ulaya bado linaendelea.

Eneo hilo la Zaporizhzhia limeshuhudia mkururo wa makombora karibu na mtambo huo, huku Moscow na Kyvi zikishutumiana kuelekeza mashambulizi katika eneo hilo la kimkakati.