Ukraine sasa yataka kuungwa mkono na Afrika
16 Mei 2022Zelensky amesema habari juu ya mahitaji ya nchi yake zinapaswa kutangazwa katika nchi zote muhimu kwa Ukraine na kwa ajili hiyo rais huyo wa Ukraine anakusudia kuyahutubia mabunge ya nchi zote za Afrika na Asia.
Ameeleza kuwa nchi yake inachukua kila hatua ili kuihamasisha dunia juu ya uvamizi wa Urusi.
Tangu Ukraine ivamiwe na majeshi ya Urusi mnamo mwezi Februari rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekuwa anayahutubia mabunge ya nchi mbalimbali duniani kote.
Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba yupo mjini Brussels ambapo atakutana na mawaziri wa Umoja wa Ulaya.
Nchi za Umoja wa Ulaya zinatarajiwa kuidhinisha msaada zaidi wa kijeshi wa euro milioni 500 kwa Ukraine, baada ya mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell kupendekeza mnamo siku ya Ijumaa.