MigogoroUlaya
Ukraine yasema imedungua droni 59 na makombora ya Urusi
8 Mei 2024Matangazo
Kupitia ukurasa wa Telegram, jeshi hilo limesema kuwa Urusi ilifanya mashambulizi 76 ya anga, kwa kutumia makombora 55 na droni 21 na kwamba mfumo wake wa ulinzi wa anga ulifanikiwa kuzuia makombora 39 na droni 20.
Soma pia: Ukraine yadai kutibua njama ya Urusi kumshambulia Zelensky
Hata hivyo, mamlaka imeeleza kuwa mashambulizi hayo yamesababisha majeruhi ya watu watatu - wawili karibu na eneo la mji mkuu Kyiv na mwengine mmoja katika mkoa wa kati ya Kirovograd.
Soma pia: Urusi yadai kuchukua udhibiti wa kijiji cha Ukraine
Hivi karibuni, Urusi imezidisha mashambulizi dhidi ya vituo vya nishati vya Ukraine na kusababisha kukatika kwa umeme na kuathiri mgao wa nishati nchini Ukraine.