1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yapokea ahadi zaidi za kupatiwa silaha

15 Juni 2023

Ukraine itapokea msaada ziada wa mifumo ya ulinzi na makombora kutoka kwa Marekani, Uingereza, Uholanzi na Denmark ili kuisadia kupambana na vikosi vya Urusi.

https://p.dw.com/p/4ScMP
Wolodymyr Selenskyj
Picha: John Moore/Getty Images

Ukraine itapokea msaada ziada wa mifumo ya ulinzi na makombora kutoka kwa Marekani, Uingereza, Uholanzi na Denmark ili kuisadia kupambana na vikosi vya Urusi.

Hayo yametangazwa leo kupitia taarifa ya pamoja ya mataifa hayo manne iliyotolewa kabla ya kuanza kwa mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.Taarifa hiyo imesema upelekaji zana hizo mpya utaanza haraka iwezekanavyo na utakamilika ndani ya muda wa wiki chache.

Mapema leo asubuhi Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg alizungumzia matarajio ya kutolewa ahadi mpya za kuipatia silaha zaidi Ukraine wakati wa mkutano wa mawaziri wa jumuiya hiyo mjini Brussels.

Mkutano huo wa NATO utafuatiwa na mwingine wa kundi la mataifa rafiki wa Ukraine linaloongozwa na Marekani unaotazamiwa kukusanya ahadi nyingine kwa serikali mjini Kyiv.