1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine: Uamuzi wa Marekani utabadili mwelekeo wa vita

19 Novemba 2024

Ukraine imesema hatua ya Marekani kuiruhusu kutumia makombora ya masafa marefu kutaisaidia Kiev.

https://p.dw.com/p/4n8X8
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andriy Sybiha
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andriy SybihaPicha: Angela Weiss/AFP/Getty Images

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andriy Sybiha amesema uamuzi wa rais wa Marekani Joe Biden wa kuiruhusu Ukraine kuishambulia Urusi kwa kutumia makombora ya masafa marefu yaliyotolewa na Marekani, unaweza kuwa msukumo mkubwa kwa Kyiv na unaweza  kubadili mwelekeo wa vita.

Waziri Sybiha amesisitiza kuwa kadiri Ukraine inavyoweza kushambulia, ndivyo vita vitakavyopungua. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amepongeza uamuzi huo wa Marekani na kusema ni hatua "nzuri kabisa" ya Washington. Naye Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema nchi yake haitochukua hatua kama hiyo.

Urusi kwa upande wake imesema itajibu vikali ikiwa makombora hayo yatatumiwa kuishambulia ardhi yake huku ikimlaumu rais wa Marekani Joe Biden kwamba hatua yake inalenga kuzidisha vita nchini Ukraine na kuchochea mvutano zaidi. Hayo yanajiri wakati leo hii Ukraine inaadhimisha siku 1,000 tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi rasmi nchini humo.