SiasaUkraine
Ukraine na Urusi zadai kuzima mashambulizi ya droni
3 Novemba 2023Matangazo
Mashambulizi hayo yalilenga mji wa pili kwa ukumbwa nchini Ukraine wa Kharkiv. Gavana wa mkoa huo Oleh Synehubov amesema mashambulizi hayo yalilenga miundombinu ya kiraia, wakati kukiwa na wasiwasi juu ya kuongezeka kwa mashambulio dhidi ya miundombinu ya nishati ya Ukraine wakati wa msimu huu wa baridi.
Kwa upande wake Urusi imetoa taarifa ambayo haikuweza kuthibitishwa kuwa imedungua pia droni 29 za Ukraine karibu na kinu kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya cha Zaporizhzhya na kuzima mashambulio matano katika rasi ya Crimea.