1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine inajiandaa na majadiliano ya kujiunga na EU

25 Juni 2024

Ukraine inatarajiwa kuanza rasmi majadiliano ya uanachama wa Umoja wa Ulaya katika kile Rais Volodymyr Zelenskyy ameelezea kama ndoto iliyotimia kwa raia wa taifa lake.

https://p.dw.com/p/4hU5e
Volodymyr Zelensky
Ukrane inajiandaa na majadiliano ya kujiunga na EUPicha: Alessandro Della Valle/POOL/AFP/Getty Images

Naibu waziri mkuu anaushughulikia ushirikiano wa Ulaya na Ulaya na Atlantiki Olga Stefanishyna ataongoza ujumbe wa Ukraine katika katika mkutano wa  Luxembourg kuashiria ufunguzi rasmi wa mazungumzo na kuoanisha sheria na viwango vya nchi hiyo na vile vya mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya.

Urusi yaishutumu Marekani kuhusika na shambulizi la Crimea

Saa chache baadae, Moldova, ambayo iliomba kujiunga na Umoja wa Ulaya baada ya Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine Februari 2022 na kupewa fursa ya kuwa mgombea miezi minne baadae, itashiriki katika kongamano tofauti baina ya serikali kuzindua rasmi mchakato wa kujiunga kwake.