1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine imepokea mkopo kutoka kwa nchi za Umoja wa Ulaya

21 Desemba 2023

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen, amesema kiasi cha Euro bilioni 1.5 za mwisho katika mpango wa msaada kwa Ukraine zimetolewa kwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4aSDa
Europäischer Union Leaders Summit: Diskussion unter EU-Führungskräften in Brüssel 2023
Picha: Jonathan Raa/NurPhoto/picture alliance

Wanachama wa nchi za Umoja wa Ulaya walikubaliana mwezi Desemba mwaka jana juu ya msaada jumla wa euro bilioni 18 kwa Ukraine.

Haijulikani jinsi msaada wa Umoja wa Ulaya  kwa Ukraine utakavyoendelea mwaka ujao, baada ya mpango mpya wa msaada wa thamani ya euro bilioni 50 kupingwa ba Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán wiki iliyopita.

Hungary yazuia msaada wa mabilioni ya dola kwa Ukraine

Mkutano maalum wa kilele wa Umoja wa Ulaya kuhusu kuendelea kuisaidia Ukraine umepangiwa kufanyika tarehe mosi mwezi Februari mwaka ujao.

Ukraine ina hadi miaka 35 ya kulipa fedha hizo, kuanzia mwaka 2033. Gharama za riba zitalipwa na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.