1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukiukwaji haki za binadamu watia mashaka Sudan

11 Februari 2013

Umoja wa Mataifa unasema serikali ya Sudan italazimika kuchukua hatua ya kushughulikia madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na vikosi vyake vya usalama.

https://p.dw.com/p/17cBK
Sudan's President Omar al-Bashir attends the African Union summit in Addis Ababa, Ethiopia, Sunday, July 15, 2012. Delegates at the African Union summit are likely to focus attention on continuing hostilities between Sudan and the year-old state of South Sudan. (Foto:Elias Asmare/AP/dapd)
Sudan Addis Abeba - Treffen der Afrikanischen UnionPicha: dapd

Kauli hiyo imetolewa na mtaalamu huru wa huo anayeshughulikia masuala ya haki za binadamu nchini Sudan baada ya kufanya ziara nchini humo siku ya Jumapili.Inadaiwa kwamba idara za usalama za Sudan zinawashikilia vigogo wa kisiasa kutoka vyama vya Upinzani pamoja na watu wengine bila ya kuwafungulia mashitaka.

Mtaalamu huyo kutoka Umoja wa Mataifa Mashood Adebayo Baderin akizungumza na waandishi wa habari ametilia mkazo kwamba ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na shirika la ujasusi la Sudan NISS unawatia mashaka wawekezaji wengi walioko ndani ya Sudan na ambao alikutana nao akiwa katika ziara yake nchi humo na kuiomba serikali kulishughulikia kwa makini tatizo hilo.

Jeshi la Umoja wa Mataifa katika UNAMID katika jimbo la Darfur
Jeshi la Umoja wa Mataifa katika UNAMID katika jimbo la DarfurPicha: Reuters

Shirika la ujasusi NISS lawamani

Inadaiwa kwamba shirika hilo la kijasusi la Sudan limekuwa likiyakandamiza mashirika ya kiraia na kuwazuia kufikisha malalamiko yao mbele ya tume ya kitaifa inayoshughulikia masuala ya haki za binadamu iliyoko mjini Khartoum.

Ukandamizaji huo umetokea licha ya ripoti ya mwanzo ya Baderin iliyopendekeza kwamba serikali ya Sudan ijenge mazingira mazuri na bora kwa mashirika ya kiraia.Wanahakati nchini Sudan wanasema mashirika matatu ya kutetea haki za binadamu ya Sudan pamoja na makundi ya kitamaduni yamepigwa marufuku au kufutiliwa mbali nchi humo suala ambalo linaongeza wasiwasi juu ya uhuru wa kujieleza.

Hata hivyo serikali inasema kwamba inayapa umuhimu mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanajishughulisha kuwasaidia wananchi pasi na kujiingiza katika agenda za kisiasa.Itakumbukwa kwamba kumekuwa kukijitokeza maandamano katika mji mkuu Khartoum yaliyotiwa nguvu na harakati za mapinduzi zilizoshuhudiwa kuanzia Misri Libya na Tunisia ambako viongozi wa huko walitimuliwa madarakani kwa nguvu ya umma, ambapo wanaharakati wakijaribu kumpinga rais Omar Hassan al-Bashir.

Serikali yaaswa kuheshimu haki za binadamu

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa,Baderin ambaye kazi yake inatambulika chini ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa pia ameitolea mwito serikali ya mjini Khartoum kuheshimu haki ya kukusanyika watu,uhuru wa kijieleza na uhuru wa uandishi habari pamoja na kuruhusu mjadala wazi wa kisiasa wakati nchi hiyo ikiandaa katiba mpya.

UN Secretary General Ban Ki-moon looks on prior to address the twenty-first session of the UN Human Rights Council on September 10, 2012 at the United Nations offices in Geneva. Ban and his human rights chief Navi Pillay called for more accountability for the bloodshed in Syria. AFP PHOTO / FABRICE COFFRINI (Photo credit should read FABRICE COFFRINI/AFP/GettyImages)
-Picha: Getty Images

Aidha mjumbe huyo amezungumzia wasiwasi wake juu ya kukamatwa vigogo wa kisiasa na watu wengine hatua inayofanywa na vyombo vya usalama.Mjumbe huyo alipata wasaa wa kukutana pia na maafisa wa serikali wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo kuwa ya kiraia wakati alipotembelea mjini Khartoum na katika jimbo la Darfur ambnako uasi umekuwa ukiendelea kwa miaka 10.

Itakumbukwa kwamba mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa alizuiwa katika ziara yake ya mwanzo kuingia jimboni Darfur kinyume na wakati huu ambapo amekubaliwa kufikifa kaskazini mwa Darfur katika mji mkuu wa jimbo hilo El Fasher na kambi inayowapa hifadhi zaidi ya watu milioni 1 walioachwa bila makaazi kufuatia mzozo wa Darfur.

Akizungumzia kile alichojionea katika eneo hilo Baderin amefahamisha kwamba usalama na hali ya haki za binadamu bado ni suala la kutiliwa mashaka lakini kuna hatua ndogo iliyopigwa katika kuimarisha hali hiyo katika kipindi cha miaka kadhaa.Mjumbe huyo anategemwa kufanya ziara yake nyingine katika eneo la Kordofan Kusini na Blue Nile ambako watu wanaokadiriwa kufikia 900,000 wameathirika kutokana na mapigano katika mikoa yote miwili ambako uasi uliibuka katika mwaka 2011.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Mohammed AbdulRahman.