1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UKAWA yapinga kura ya maoni ya Katiba Mpya

Bruce Amani22 Oktoba 2014

Umoja wa Katiba ya Wananchi nchini Tanzania (UKAWA) umeikosoa hatua ya serikali ya nchi hiyo kutangaza kura ya maoni ya katiba iliyopendekezwa hapo Aprili 2015, likisema hakuna matayarisho.

https://p.dw.com/p/1DZwH
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari.Picha: DW/M.Khelef

Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi (CUF), moja ya vyama vinavyounda umoja huo, anasema kweye mahojiano haya na Bruce Amani wa Idhaa ya Kiswahili ya DW kwamba kuna mapungufu mengi kwenye mchakato mzima wa kupatikana kwa Katiba Mpya na pia ukosefu wa uwezo wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) mbali na kukosekana kwa maridhiano ya kitaifa kuelekea hatua hiyo muhimu na ya kihistoria.

Kusikiliza mahojiano kamili, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Mohammed Khelef