Ukame wazidi kuathiri mamilioni Pembe ya Afrika
17 Julai 2011Matangazo
Mkurugenzi Anthony Lake amesema, mvua hazitazamiwi kunyesha karibuni na msimu wa mavuno unakaribia. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, maelfu ya watu wameondoka Somalia kwa sababu ya ukame ulioathiri pia mamilioni ya watu na kuteketeza mifugo katika nchi jirani za Kenya,Ethiopia na Djibouti. Ujerumani imeahidi kutoa Euro milioni 5 kuwasaidia wahanga wa ukame katika kambi za ukimbizi.