1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukahaba watishia maisha ya watoto Kenya

Thelma Mwadzaya20 Desemba 2006

Unyanyasaji wa kijinsia wa watoto umefikia viwango vya kushtua hasa katika wale wa umri wa miaka 12 hadi 18.Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Shrika la Umoja wa Mataifa la watoto UNICEF iliyochapisha mwanzoni mwa wiki.

https://p.dw.com/p/CHlq
Unicef yachapisha ripoti inayoelezea ukahaba kwa watoto Kenya
Unicef yachapisha ripoti inayoelezea ukahaba kwa watoto Kenya

Utafiti huo ulidumu kwa mwaka mmoja katika mkoa wa pwani na kudhihirisha kuwa asilimia 30 ya wasichana wadogo wanahusika na vitendo vya ukahaba.

Utafiti huo uliofanyika katika wilaya za Kwale,Kilifi,Malindi na Mombasa ulibaini kuwa takriban wasichana alfu 15 wanahusika na ukahaba vilevile wengine alfu 2 wakijumuisha vijana wanahusika na shughuli hiyo kila siku.

Utafiti huo unaelezea ukubwa wa tatizo hilo na athari zake hasa katika watoto wanaonyanyaswa kijinsia katika eneo la pwani nchini Kenya.Ukahaba unakiuka haki za watoto katika eneo hilo aidha kuweka bayana matatizo yanayowakumba watoto nchini Kenya.

Kulingana na ripoti hiyo matatizo ya pesa na umasikini ndio vyanzo vya shughuli hiyo ya ukahaba hasa kwa watoto.Utafiti huo aidha umevumbua kuwa watoto kutoka maeneo mengine ya nchi mbali na yale ya pwani nao huhusika kabla kuwasili.

Kwa mujibu wa mwandishi wa ripoti hiyo Sara Jones wengi wao hawatumii mipira ya kondom.