1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yaahidi msaada usio na kikomo kwa Ukraine

4 Oktoba 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amewaambia viongozi wamataifa ya G7 na Jumuiya ya Kujihami NATO kwamba taifa lake lipo tayari kuisadia Ukraine vitani kwa kadri itakavyowezekana.

https://p.dw.com/p/4X5Ae
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak kwenye picha ya pamoja na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy mjini Vilnius, Lithuania
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak kwenye picha ya pamoja na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy mjini Vilnius, LithuaniaPicha: Paul Ellis/AP/picture alliance

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amewaambia viongozi wa mataifa saba yaliyoendelea zaidi kiviwanda duniani, G7 na Jumuiya ya Kujihami NATO kwamba taifa lake lipo tayari kuisadia Ukraine vitani kwa kadri itakavyowezekana.

Taarifa ya ofisi yake imeyataja maeneo ya msaada huyo kuwa ni pamoja na ya kiutu na uchumi pamoja na kusisitiza kuwa msaada huo utaendelea kadri vita hivyo vinavyoendelea.

Wito huo umepokelewa vyema Rais wa Marekani Joe Biden pamoja na changamoto ya bunge la taifa lake kuzuia mswada wa usaidizi huo kwa Ukraine kwa lengo la kunusuru utendaji wa serikali.