Ujumbe wa viongozi wa Afrika kukutana na rais Putin wa Urusi
17 Juni 2023Matangazo
Timu hiyo ya kidiplomasia ilikuwa Kyiv jana Ijumaa kueleezea mashaka yanayolikumba bara la Afrika kutokana na uvamizi wa Urusi nchini humo, na hasa kupanda kwa bei za nafaka, huku rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akisisitizia umuhimu wa amani kwa njia ya mazungumzo.
Hata hivyo Zelensky aliondoa uwezekano huo katika mkutano pamoja na waandishi wa habari na kurudia matamshi aliyoyatoa mara kadhaa kwamba kuingia makubaliano na Urusi kwa sasa kutamaanisha kusitisha kwa muda vita, mateso na machungu.
Zelensky badala yake ameliomba kundi hilo linalohusisha marais wanne kutoa mitizamo yao juu ya namna ya kumaliza uhalifu uliofanywa na Urusi na kushughulikia suala la upatikanaji wa chakula cha kutosha.