Ujumbe wa pamoja wa maafisa wa ngazi za juu kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika umekamilisha ziara rasmi nchini Somalia jana Jumatano na kuhimiza serikali ya nchi hiyo kuwashirikisha kwa dhati wanawake katika maswala ya amani, usalama na maendeleo.