1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa Saudi Arabia upo Iran

10 Aprili 2023

Ujumbe wa serikali ya Saudi Arabia umewasili mjini Tehran, Iran, katika jitihada ya mataifa hayo hasimu ya muda mrefu ya kusaka namna ya kujongeleana tena.

https://p.dw.com/p/4PsbF
China Peking | Treffen der Außenminister von Iran und Saudi-Arabien | Hossein Amir-Abdollahian und Prinz Faisal bin Farhan Al Saud
Picha: Iran's Foreign Ministry/WANA/REUTERS

Ujumbe wa serikali ya Saudi Arabia umewasili mjini Tehran, Iran, katika jitihada ya mataifa hayo hasimu ya muda mrefu ya kusaka namna ya kujongeleana tena.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia, ujumbe huo ulijadili kufunguliwa tena kwa ubalozi wa Saudia mjini Tehran na ubalozi mdogo kwenye mji mwingine wa Mashhad ulioko kaskazini mashariki mwa Iran.

Kwa muda mrefu, Saudi Arabia yenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Sunni na Iran yenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia hazikuwa na mahusiano ya kidiplomasia. Mataifa yote yanapigania ushawishi wa kisiasa na kijeshi wa kikanda.