Ziara hiyo ni muhimu kwani inajiri siku nne tu baada ya kushindwa kwa utekelezwaji hatua ya kusitisha vita baina ya jeshi la Kongo (FARDC) na waasi wa M23 ambao Kinshasa inawataja kuwa magaidi na ambao Umoja wa mataifa tayari umetambua wanaungwa mkono na Rwanda. Baraza la Usalama halijaitembelea Kongo tangu mwaka 2018.