Ujia wa Maji wa Hormuz. Guba la Uajemi: Meli ya mafuta ya Japan na nyambizi ya Kimarekani zinagongana katika ujia wa Hormuz katika Bahari ya Waarabu.
9 Januari 2007Matangazo
Meli ya kubea mafuta ya Japan na nyambizi ya Kimarekani inayokwenda kwa nguvu za kinyukliya zimegongana katika Bahari ya Waarabu, karibu na ujia wa maji wa Hormuz. Wizara ya mambo ya kigeni ya Japan ilisema hakujakuweko na majeruhi wala hamna mafuta yaliomwagika baharini. Jeshi la Marekani lilisema nyambizi yao, kwa jina la USSNewport News, haijaharibika. Meli ya kubebea mafuta ya Japan ilikuwa inaelekea Singapore.