1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yayaonya makampuni yanayokwepa vikwazo vya Urusi

12 Aprili 2023

Naibu Kansela wa Ujerumani ambaye pia ni waziri wa uchumi Robert Habeck amesema serikali ya nchi hiyo ni lazima ichukue hatua kali dhidi ya kampuni zinazokiuka vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4PqCA
Habeck will Umgehung von Russland-Sanktionen erschweren
Picha: Wolfgang Kumm/picture alliance/dpa

Katika mahojiano na magazeti kadhaa yaliyochapishwa leo, Habeck amesema wale wanaokwepa vikwazo dhidi ya Urusi wakitumia mbinu ya uwakala kupitia nchi nyingine wanapaswa kuadhibiwa.

Tangu Urusi ilipotuma majeshi yake nchini Ukraine mwaka uliopita, Umoja wa Ulaya umetangaza awamu 10 ya vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Moscow ikiwemo vizuizi vikali vya kufanya biashara na dola hiyo.

Hata hivyo kumekuwepo ripoti kuwa baadhi ya kampuni barani Ulaya zinakwepa vikwazo hivyo kwa njia za kinyemela, mwenendo unaotishia kuvuruga malengo ya kuwekwa vizuizi hivyo.