Ujerumani yatoa wito wa kupunguzwa mivutano ya China, Taiwan
13 Aprili 2023Ziara hii ya Baerbock inakuja kufuatia mazoezi ya kijeshi ya China karibu na kisiwa hicho kilicho na utawala wa ndani ambacho China inadai ni sehemu ya himaya yake.
Wizara ya ulinzi ya Ujerumani imesema miongoni mwa mambo atakayoyajadili baerbock ni mivutano ya Taiwan, vita vya Ukraine na masuala ya haki za binadamu.
Chama tawala cha Kikomyunisti huko China kilipeleka meli na ndege za kivita karibu na Taiwan mwishoni mwa wiki iliyopita kama jawabu la mkutano kati ya spika wa bunge la Marekani Kevin McCarthy na rais wa Taiwan Tsai Ing-wen.
Serikali za Ulaya zinazidi kuhofia shinikizo la China kwa Taiwan. Baerbock pia anapanga kusafiri kuelekea Korea Kusini mnamo siku ya Jumamosi na baadae kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G7 huko Japan.