Ujerumani yatinga nusu fainali
5 Julai 2014Beki huyo wa Borussia Dortmund aliruka juu na kupachika wavuni mpira kutokana na krosi ya free kick iliyochongwa na Toni Kroos katika dakika ya 13 na kutuliza mambo katika uwanja wa Maracana. Ufaransa walianza mchezo wa kujikokota na kuwapa nafasi Ujerumani kutawala mambo uwanjani katika kipindi cha kwanza. Katika kipindi cha pili Ufaransa walireeja kwa kishindo wakati Hummels akiiokoa Ujerumani kwa kuzuia shuti iliyopigwa an Karim Benzema, muda mfupi kabla ya mlinda lango Manuel Neuer kulipangua kombora lililovurumishwa na Blaise Matuidi.
Kocha Löw alibadilisha mbinu zake kwa mara ya kwanza nchini Brazil, alipomhamisha nahodha Philipp Lahm kutoka katikati ya uwanha na kumweka katika nafasi yake ya zamani ya beki wa kulia, huku BASTIAN Schweinsteiger na Sami Khedira wakishirikiana katikati mwa uwanja kama viungo. Miroslav Klose alipewa ruhusa ya kuanza kama mshambuliaji kwa mara ya kwanza tangu dimba hilo lilipoanza. Hummels alichukua nafasi ya Metersacker kama beki wa katikati baada ya kuukosa mchuano ambao waliishinda Algeria magoli mawili kwa moja kutokana na maumivu. Ujerumani inakutana na mshindi wa mechi nyingine ya robo fainali kati ya wenyeji Brazil na Colombia inayochezwa mjini Fortaleza.
Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AP
Mhariri: Daniel Gakuba