1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatamba 4:0 mbele ya Australia

Josephat Nyiro Charo14 Juni 2010

Kikosi cha kocha Joachim Löw kimedhihirisha umariri wake wa kusakata ngozi ya"Jabulani" kwa ustadi mkubwa

https://p.dw.com/p/Nq35
Miroslav Klose, wa pili kutoka kulia, akimkumbatia mwenzake, Per Mertesacker, wa tatu kushoto, baada ya mechi yao na AustraliaPicha: AP

Katika mashidano ya kuwania kombe la dunia nchini Afrika Kusini, Ujerumani imeshinda mechi yake ya kwanza kwa kuichabanga Australia mabao manne kwa bila.

Washambuliaji, Lukas Podolski na Miroslav Klose waliliona lango la Australia katika dakika 30 za kwanza.

Magoli mawili ya Ujerumani yaliongezwa katika kipindi cha pili cha mchezo, na Thomas Müller na Cacau.

Hata hivyo katika kipindi cha pili Australia ilibakiwa na wachezaji 10 baada ya Tim Cahill kuonyeshwa kadi nyekundu kwa sababu ya kucheza faulo.

Hapo awali Ghana iliibwaga Serbia kwa bao moja la penalti baada mchezaji wa Serbia kuunawa mpira ndani ya eneo nyeti katika dakika ya 86.

Kabla ya mechi hiyo Slovenia ijipatia ushindi wa kwanza katika mshindano ya kombe la dunia kwa kuifunga Algeria bao moja kwa bila.