Ujerumani yatahadharishwa kushambuliwa na al-Qaeda.
13 Januari 2008Beirut. Maafisa wa Lebanon wamewaeleza maafisa wa Ujerumani kuwa wanaamini kuwa watu wenye imani kali wanapanga kufanya shambulizi la kigaidi nchini Ujerumani. Tahadhari hiyo imesababisha wizara ya sheria kuimarisha hatua za kiusalama nchini Ujerumani. Maafisa wamesema kuwa wamepewa tahadhari hiyo baada ya maafisa wa Lebanon kumkamata mtu mmoja anayesadikiwa ni mshirika wa kundi la kigaidi la al-Qaeda mjini Beirut. Mtuhumiwa huyo anaaminika kuwa ameupigia simu ubalozi wa Ujerumani mjini Beirut mapema wiki hii, akidaiwa kuwa ametishia kufanya shambulizi katika maeneo ya kiusalama ya Ujerumani kwa kulipiza kisasi kwa ajili ya kuhukumiwa mtuhumiwa wa kundi la al-Qaeda nchini Ujerumani.