Ujerumani yasema mazungumzo ya Gaza hayapaswi 'kuhatarishwa'
6 Mei 2024Matangazo
Hayo yanajiri baada ya tofauti kuzidi kuongezeka baina ya Israel na Hamas katika mazungumzo ya mwishoni mwa juma mjini Cairo.
Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imesema mazungumzo hayo hayapaswi kudhoofishwa, na pande zote lazima zifanye juhudi kubwa kuhakikisha kuwa watu wa Gaza wanapewa misaada ya kibinadamu na mateka wanaachiliwa.
Kauli ya Ujerumani inatolewa, mnamo wakati Israel ikiamuru kuanza kuondolewa kwa Wapalestina kutoka mjini Rafah mapema siku ya Jumatatu.
Israel kwa muda mrefu imetishia kufanya mashambulizi ya ardhini katika mji huo, hali iliyozua taharuki kubwa duniani.
Katika hatua nyingine, Ujerumani imekosoa uamuzi wa Israel wa kuzuia kituo cha habari cha Al Jazeera na kutaka kulindwa kwa uhuru wa vyombo vya habari.