Ujerumani yasema itaiunga mkono Ugiriki
16 Januari 2012Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle ameihakikishia serikali ya Ugiriki kuwa Ujerumani itasimama pamoja na Ugiriki. Katika ziara yake nchini Ugiriki , alikutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Lucas Papademos pamoja na waziri wa mambo ya kigeni Stavros Dimas.
Westerwelle ameweka wazi kuwa Ugiriki ina nafasi katika bara la Ulaya. Westerwelle pia amesema kuwa huu ndio wakati ambao bara la Ulaya linapaswa kushughulikia hatua ya mashirika ya kuweka viwango vya ukopaji na kutuliza masoko.
Akizungumza kwa lugha ya kiingereza kusisitiza suala hilo, ametilia mkazo kuwa makubaliano na mikataba iliyofikiwa na mataifa wanachama wa umoja wa Ulaya inahitaji kupewa nafasi ili kufanyakazi.
Siku ya Ijumaa , shirika la Standard and Poors lilishusha viwango vya mataifa tisa ya Ulaya , miongoni mwao ikiwa ni Ufaransa, ambayo imepoteza alama yake ya juu ya A tatu.