1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yapewa darasa na Hungary na Ureno yatumai kuvuna Euro milioni 262 kutoka kombe la ulaya.

Ramadhan Ali7 Juni 2004
https://p.dw.com/p/CHaH
Kipa wa Ujerumani Kahn akiondoka uwanjani shingo upande
Kipa wa Ujerumani Kahn akiondoka uwanjani shingo upandePicha: AP

Tuanze na Kombe la Ulaya la mataifa baada ya jana timu kadhaa za Ulaya kumaliza changamoto zao za kujipima nguvu-Ujerumani ikichezeshwa kindumbwe-ndumbwe na Hungary na kuchapwa mabao 2:0 tena nyumbani.

Ureno yenyewe –mwenyeji wa Kombe hili inatumai kuvuna kitita cha dala 323 zaidi kutokana na watalii watakaomiminika nchini-hii ni kwa muujibu wa makadirio ya serikali.Ureno inatarajia kiasi cha watalii nusu-milioni kuingia nchini kwa Kombe la Ulaya linaloanza jumamosi hii Juni 12 hadi finali Julai 4.

Kwa mfano watalii 50.000 kutoka urusi wanatarajiwa huko Algarve,kwenye pwani na ambako hoteli hazitamudu kuwakirimu watalii wote na pia kutokana na bei zake za juu. Hatahivyo, mashabiki 12.000 hadi sasa wamethibitisha kuwasili Algarve.

Kombe la Ulaya 2004 linatarajiwa kuvutia watazamaji 1.2 milioni viwanjani na wengine bilioni 9 kupitia TV. Kabla firimbi basi kulia jumamosi hii,makamo-bingwa wa dunia-Ujerumani waliingia jana uwanjani huko Kaiserslauten kupasha moto mashini yao mbele ya wahungary.Timu hizi 2 zilöikumbana katika finali ya Kombe la dunia 1954 mjini Berne,Uswisi zama ambazo Hungary ikitikisa dimba barani Ulaya ikicheza na stadi wake Puskas.Ingawa Ujerumani iliifunga Hungary kwa mastaajabu katika finali 3-2 baada ya hungary kuongoza 2:0,ushindi huo uliipatia Ujerumani kombe lake la kwanza la dunia.

Jana lakini mambo yalikua tofauti.Hungasry iliikomea Ujerumani mabao 2:0 na hii ikapunguza matumaini ya mashabiki wa Ujerumani kutwaa kombe la Ulaya huko Ureno.Ujerumani imeangukia kundi na inafungua dimba katika kundi lake na Holland.Mahasimu wengine katika kundi hili ni Jamhuri ya Czech na Latvia. Mbele ya holland,Ujerumani haitapata mteremko na huo ndio mpambano unaosubiriwa kwa hamu kuu. Kocha wa hungary jana alikua nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani Lothar Matthaus ambae ameichezea Ujerumani mara 150.

Licha ya pigo alioipa Ujerumani jana,Matthaus anadai kuwa Ujerumani ina ustadi mkubwa na anahisi kuwa inaweza alao kuwasili nusu-finali.Anakumbusha kuwa katika Kombe la dunia lililopita, Ujerumani kwanza ililazwa bao 1:0 na Wales kabla haikufululiza njia yake kupitia Kamerun na kuingia finali ya kombe la dunia kati yake na Brazil.

Taarifa kutoka Frankfurt makao makuu ya Shirikisho la dimba la Ujerumani, yanasema miji ifuatayo ya Ujerumani itachezewa Kombe la mashirikisho-Confederations Cup hapo juni 15 hadi 29 mwakani-mwaka kabla kluanza Kombe la dunia .Miji yenyewe ni Frankfurt,Cologne,Hannover,Leipzig na Nüremberg.Kila mmoja kati ya miji hiyo 5 utaandaa mechi 3 isipokua Frankfurt utakaoandaa mechi 4.Timu 4 kati ya 8 zitakazoshiriki zitaangukia kundi 1 na wenyeji Ujerumani,m,abingwa wa dunia Brazil,Tunisia mabingwa wa mwaka huu wa Afrika,mabingwa wa mwaka huu wa Amerika Kusini,mabingwa wa eneo la Oceania na mshindi wa Kombe la Ulaya la Mataifa mwaka huu nchini Ureno.Ikiwa lakini Brazil imeibuka bingwa wa Copa Amerika-Kombe la Amerika kusini,basi nafasi yake itachukuliwa na timu itakayoibuka m akamo-bingwa.Hali itakua hivyo hivyo endapo Ujerumani ikiibuka mabingwa wa Ulaya nchini Ureno.