1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yanuwia kudhibiti uhalifu wa kutumia visu

12 Aprili 2023

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser anasema atachukua hatua kali zaidi kukabiliana na uhalifu wa kutumia visu.

https://p.dw.com/p/4PxXP
Treni ya mwendokasi nchini Ujerumani
Matukio ya uhalifu wa kutumia visu nchini Ujerumani huripotiwa sana mitaani na kwenye vyombo vya usafiri Picha: Vifogra/AP Photo/picture alliance

Mpango wake unakuja siku chache baada ya rais wa Shirikisho la Polisi kutoa wito huo kwa maeneo yasiyo na silaha ndani na karibu ya vituo vya treni na katikati mwa jiji. 

Suala la uhalifu wa kutumia visu lilirejea nchini Ujerumani baada ya watu wawili kuuawa na saba kujeruhiwa katika shambulio kwenye treni iliyokuwa ikisafiri kutoka Kiel kwenda Hamburg mwezi Januari mwaka huu.

Mwezi Desemba 2022, msichana mmoja mwenye umri wa miaka 14 alifariki na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kuvamiwa na mwanamme aliyekuwa na kisu walipokuwa wakielekea shuleni katika kijiji cha Illerkirchberg kusini mwa Ujerumani.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni za uhalifu, kulikuwa na mashambulizi 8,160 ya visu mwaka 2022, ongezeko la asilimia 15.4 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Lakini Ofisi ya Shirikisho la Polisi ya Jinai BKA haikuchapisha takwimu zozote za uhalifu wa kutumia visu hadi kipindi cha mwaka 2021 ambapo kulikuwa na  vizuizi vya UVIKO-19.

Takwimu zinaashiria ongezeko la uhalifu wa kutumia visu 

Polisi wakiwa mjini Brokstedt
Mkasa wa shambulizi la kutumia kisu huko Brokstedt uliwashtua wengi nchini UjerumaniPicha: FABIAN BIMMER/REUTERS

Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa idara ya polisi GdP, Jochen Kopelke, amesema takwimu hizo ni uthibitisho kwamba uhalifu wa kutumia visu unazidi kuwa tatizo la nchi nzima.

Shirikisho hilo liliripoti kwamba idadi ya mashambulizi ya visu yameongezeka mara mbili zaidi kutoka 46 hadi 98 kati ya nusu ya pili ya mwaka 2021 na nusu ya kwanza ya 2022 na kwamba vizuizi vya kusafiri vilivyowekwa kwa sababu ya UVIKO-19 vimesababisha kuchangia ongezeko hili.

Kwa upande wake Marcel Emmerich ambaye ni Mbunge wa Chama cha Kijani na mwenyekiti wa kamati ya sera ya mambo ya ndani ya bunge, amesema licha ya tahadhari kwa umma kuhusu suala hilo lakini data za msingi hazionyeshi kwamba uhalifu wa visu umeongezeka.

Kulingana na Rausch, unyanyasaji mwingi wa kutumia visu hutokea majumbani huku ukihusishwa na pombe, dawa za kulevya na hali ya msongo wa mawazo mara nyingi hutokea katika  katika mazingira ya nyumbani au ya maeneo yenye mikusanyiko ya watu.

Majimbo yaanza kuchukua hatua kunusuru maisha 

Idadi ya miji ya Ujerumani tayari imeanzisha maeneo yasiyo na silaha, katika maeneo ya Cologne, Düsseldorf, Rhine Kaskazini-Westphalia, mtu yeyote atakayepatikana amebeba bunduki ya kustaajabisha, kisu chenye ncha ndefu zaidi ya sentimeta 4 (inchi 1.5), gesi ya machozi au dawa ya pilipili atakabiliwa na faini ya hadi Euro10,000.

Takriban silaha 350 zimekamatwa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, ikiwa ni pamoja na visu vya kipepeo, daga, blau za kubadilishia umeme, virungu vya darubini, dawa zenye pilipili , na bastola na mabomu ya machozi.

Mnamo Septemba mwaka jana, serikali ya jimbo la Baden-Württemberg ilitangaza kwamba miji ya manispaa itaweza kuanzisha maeneo yasiyo na silaha katika maeneo yenye uhalifu.

Jimbo hilo la kusini-magharibi lilikuwa limesajili uhalifu wa kutumia visu 14,900 mwaka wa 2021, huku uhalifu wa kutumia visu ukiwa ni uhalifu mmoja kati ya kumi ya uhalifu wa kutumia nguvu kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya jimbo hilo.

Je, kuna ulegevu wa sheria katika kupambana na matumizi ya visu kama silaha?

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser Picha: Martin Müller/IMAGO

Nchini Ujerumani, sheria inayofunika umiliki wa visu hutofautiana kulingana na aina ya kisu.

Tofauti na bunduki, hakuna leseni ya kubeba au kutumia visu vilivyoainishwa kama silaha. Vitu (bila kujumuisha bunduki) vinavyoweza kutumika kusababisha jeraha kwa nguvu ya misuli kwa namna ya vipigo, visu, kurusha au misukumo huchukuliwa kuwa silaha.

Ingawa ni halali kumiliki visu vingi ambavyo viko chini ya kategoria hii, mtu hawezi kuvibeba hadharani.

Kwa kujibu ombi la gazeti la Bild am Sonntag mwezi Januari, polisi wa Ujerumani walisema kuwa wamesajili uhalifu 398,848 kwenye treni na katika vituo vya treni mwaka wa 2022 - ongezeko la 12% ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Kati ya uhalifu huo, 14,155 ulihusisha shambulio la mwili na 336 ulihusisha matumizi ya kisu - zaidi ya mara mbili mwaka uliopita.