SiasaChad
Ujerumani yamfumkuza balozi wa Chad
11 Aprili 2023Matangazo
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani, Balozi Mariam Ali Moussa, anapaswa kuondoka haraka.
Vyanzo viwili kutoka serikali ya Chad vilisema siku ya Jumamosi kwamba Balozi wa Ujerumani nchini humo, Gordon Kricke, alifukuzwa kutokana na kauli zake tete juu ya hali ya kisiasa nchini Chad.
Hata hivyo, wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani imekanusha balozi wake huyo kutenda kosa lolote lile, na badala yake imesema Balozi Kricke alikuwa akitekeleza majukumu yake ipasavyo akiwa ameshiriki kwenye mazungumzo juu ya haki za binaadamu na kurejea haraka kwa utawala wa kiraia nchini humo.